Meneja wa Klabu Bingwa nchini Hispania Real Madrid Zinedine Zidane amesema hana mpango wa kumpumzisha mshambuliaji  wake kutoka nchini Ufaransa Karim Benzema, baada ya kuwa na wakati mgumu kwenye mchezo dhidi ya Celta Vigo.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 33, hakuwa kwenye kiwango cha kawaida kwenye mchezo huo uliochezwa Jumamosi (Januari 02), huku Real Madrid wakishinda mabao mawili kwa moja.

Ni dhahir ilionekana Benzema hakuwa kwenye kiwango chake, hasa baada ya kushindwa kupiga shuti hata moja kwenye mchezo huo.

Kufuatia hali hiyo waandishi wa habari walimuuliza Zidane kama ana mpango wa kumpumzisha Benzema, ambaye amefunga mabao manane katika Ligi ya Hispania (LaLiga), meneja huyo kutoka Ufaransa aliwajibu hana mpango huo na badala yake ataendelea kumtumia kwenye michezo inayofuata.

Zidane alisema hadhani kama Benzema amachoka kama ilivyoonekana kwenye mchezo huo, ambao ulishuhudia Real Madrid wakiwa kwenye mazingiramagumu ya kupata ushindi.

 “Sidhani kama amechoka. Nadhani alifanya vizuri na nikamchukua ili mchezaji mwingine acheze. Tuko katika uelekeo mzuri. Tunafanya vitu sahihi na lazima tuendelee hivi.” Alisema Zidane.

Benzema ameanza katika michezo 15 kati ya 17 ya LaLiga msimu huu, huku mlinda mlango Thibaut Courtois pekee na beki Raphael Varane wakicheza dakika nyingi zaidi yake.

Familia ya Baba wa Taifa yatoa ratiba ya mazishi
Songani: Tuna kazi kubwa kuing'oa Simba SC