Kocha wa Klabu ya Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa haikuwa rahisi kuifunga Klabu ya Bayern Munich katika mchezo wa nusu fainali wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya.

Amesema kuwa Bayern Munich ilicheza kwa kiwango cha juu na Real Madrid ilifanya kazi ya ziada kupata ushindi wa mabao 2- 1 ugenini kwenye uwanja wa Allienz Arena.

Mchezaji Joshua Kimmich alianza kuipa presha timu ya Real Madrid baada ya kumchambua gori kipa Keylor Navas kwa kupachika goli la kuongoza.

Aidha, beki kisiki wa Real Madrid, Marcelo alipachika bao la kusawazisha kabla ya Bayern Munich kuwapoteza nyota wawili Arjen Robben na Jerome Boateng baada ya kuumia.

“Nimeridhika sana na kiwango cha wachezaji, lakini makosa yalikuwa mengi sana dakika za awali, tulitumia nguvu nyingi sana kuimudu presha ya wapinzani wetu,”amesema Zidane

CCM yakomba safu nzima ya uongozi Chadema
Singida United yaichimba mkwara Mbeya City

Comments

comments