Zinedine Zidane anatajwa kujiunga na Manchester United kuchukua nafasi ya Jose Mourinho endapo kocha huyo ataachana na timu hiyo msimu huu.

Zidane ambaye ni raia wa Ufaransa hana timu anayofundisha kwasasa baada ya kujiudhuru kuifundisha  Klabu ya Real Madrid ya nchini Hispania mapema mwaka huu anadaiwa kujiandaa kujiunga na moja ya timu kubwa kwenye ligi kuu nchini Uingereza.

Hata hivyo, hivi karibuni kumekuwepo na harufu ya Mourinho kuondoka ndani ya Klabu ya Manchester United licha ya kutokuwa na rekodi mbaya tangu alipojiunga na mashetani hao wa Old Trafford.

Tangu kuanza kwa msimu mpya wa 2018/2019 kumekuwepo na hisia kuwa United itatafuta kocha mpya na Zinedine Zidane ndiye kocha anayetajwa sana kujiunga na timu hiyo yenye mashabiki wenye kiu ya mataji.

Zidane alijiudhuru kuifundisha Madrid baada ya kuipatia mafanikio makubwa klabu hiyo ndani ya muda mfupi ikiwemo kuiongoza timu hiyo kuchukua kombe la klabu bingwa barani ulaya.

 

NEC yaviasa vyama vya siasa kufuata sheria za uchaguzi
Tanzania kinara kesi za haki za binadamu