Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ itacheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Zimbabwe ‘The Warriors’ Novemba 13, 2016 katika uwanja wa Taifa jijini Harare nchini Zimbabwe.

Stars imepata mchezo huo wa kirafiki kufuatia awali kushindwa kucheza na timu ya Taifa ya Ethiopia mwezi Oktoba.

Katika mchezo wa mwisho kati ya Zimbabwe dhidi ya Tanzania, uliochezwa mwaka 2014 timu hizi zilitoka sare ya mabao 2 – 2.

Kufuatia Zimbabwe kukubali kucheza mchezo huo na Tanzania katika kalenda FIFA itakayoanza Nov 7 – 13, Mkwasa anatarajiwa kutangaza kikosi chake wakati wowote juma hili.

Lowassa ahudhuria Kikao cha Bunge kama mgeni
Kinnah Phiri: Tupo Tayari Kuwakabili Young Africans