Polisi waliruhusu vyama vya wafanyakazi kufanya maandamano hayo ya kudai mishahara bora, jambo ambalo lilikiuka amri ya Rais Emmerson Mnangagwa, ambaye siku za hivi karibuni alipiga marufuku maandamano ya upinzani.

Serikali imesema haina uwezo wa kulipa mishahara inayoendana na thamani ya dola ya Marekani, hali ambayo itapelekea mfanyakazi anayepokea mshahara mdogo kulipwa dola ya Zimbabwe elfu 7,293, sawa na dola za Marekani 475 kwa mwezi, kuliko dola ya Zimbabwe 1,023 anazolipwa sasa.

Ikumbukwe kuwa wafanyakazi wa Zimbabwe wanaathirika kutokana hali mbaya ya uchumi wa taifa, inayosababishwa kwa kiasi kikubwa na mfumuko wa bei ya bidhaa muhimu, uhaba wa sarafu za kigeni, mafuta na dawa, pamoja na mgao wa umeme ambao unazorotesha shughuli za viwanda na uchimbaji madini.

Polisi wafanikiwa kumua jambazi 'Kambale'
AUWSA yatakiwa kuharakisha huduma ya maji Namanga