Kituo cha habari cha taifa cha Zimbabwe kimepiga marufuku kurusha mahubiri ya watu wanaojitanabaisha kuwa ni ‘manabii wa mafanikio’, wakihubiri kuhusu mafanikio ya kiuchumi na kijamii kwa waumini wa dini ya Kikristo.

Kwa mujibu wa gazeti la Daily News la nchini humo, Mkuu wa Shirika la Habari la Zimbabwe (ZBC), Albert Chekayi, amesema wameamua kusitisha matangazo ya wahubiri hao baada ya kupokea malalamiko ya wasikilizaji wengi kuhusu madhara yake.

  • Wakosoaji wa mahubiri ya aina hayo wameeleza kuwa wahubiri hao wamekuwa wakijineemesha kwa kupata kiasi kikubwa cha fedha kutoka kwa watu masikini kwa kuwaaminisha kuwa watapata mafanikio.

Wahubiri hao wamekuwa wakieleza kuwa kadiri mtu anavyozidi kutoa kwa kanisa na imani yake inavyokuwa ndivyo atakavyozidishiwa kwa kupata mafanikio zaidi na mali.

Aidha, ZBC imeeleza kuwa itafanya uchunguzi wa kina kufahamu kama madai ya baadhi ya wasikilizaji wa vipindi hivyo yana ukweli au ni ukosoaji wa masuala ya kiimani.

Majambazi walipua na kupora benki tano
Kaya 45 zaathirika na mvua mkoani Kagera