Meneja wa klabu ya Real Madrid Zinedine Zidane amekanusha kuwepo kwa mgogoro kwenye kikosi chake ambao unatajwa kusababisha matokeo ya sare yaliyowaandama katika michezo minne iliyopita.

Real Madrid jana walishindwa kufurukuta mbele ya Eibar na kujikuta wakiambulia sare ya bao moja kwa moja.

Zidane aliwaambia waandishi wa habari mara baada ya mchezo huo, hakuna jambo lolote baya linalowasibu wachezaji wake, na kinacho onekana uwanjani ni kawaida ya mchezo wa soka ambao huamuliwa na matokeo ya aina tatu, Kufungwa, Kushinda na Kutoka sare.

Alisema yanayozungumzwa kupitia baadhi ya vyombo vya habari kuhusu mkwaruzano ambao unadaiwa kukitafuna kikosi chake, amekua akiyaona na kuyasikia lakini yeye kama meneja amekua akiyapuuza.

“Hakuna baya linaloendelea kikosini, naamini ni matokeo ya kawaida ambayo yanaweza kuikuta timu yoyote duniani, hivyo sina shaka, kwani ndio kwanza tumeanza mwezi Oktoba na bado tuna michezo mingine ambayo tutahakikisha tunapambana na kupata point tatu muhimu,”

“Jambo hili la kutoka sare katika michezo minne halinipi shida kabisa, nimeona tunapokosea na nitajitahidi kuyafanyia kazi makosa yetu ili tuweze kufanikiwa.” Alisema  Zidane alipozungumza na waandishi wa habari.

Michezo minne ya Real Madrid iliyomalizika kwa matokeo ya sare

Real Madrid 1 – 1 Villarreal (La Liga)

Las Palmas 2 – 2 Real Madrid (La Liga)

Dortmund 2 – 2 Real Madrid (Ligi ya mabingwa barani Ulaya)

Real Madrid 1 – 1 Eibar (La Liga)

Arsene Wenger: Sikuona Kama Ameshika Ama Hakushika
Video: Nyoka apoteza maisha baada ya kung’ata ‘ziwa feki’ la mrembo kwenye tamasha