Mara baada ya Idara ya uhamiaji kufanya uzinduzi wa hati mpya za kusafiria, hati ya kielektroniki iliyozinduliwa na Rais John Pombe Magufuli, Uhamiaji imetoa maelekezo muhimu kwa wananchi yatakayo toa mwongozo na hatua stahiki za kuzingatiwa ili kuipata hati hiyo mpya ya kusafiria maarufu kama Pasipoti.

Ambapo Msemaji wa Uhamiaji, Ally Mtanda amesema kuwa hatua ya kwanza na muhimu mwombaji lazima awe na kitambulisho cha taifa, hivyo ameshauri kwa wale ambao bado hawana watembelee ofisia za NIDA, kwa kupata kitambulisho hicho.

Hatua ya pili mwombaji anapaswa kutembelea tovuti ya uhamiaji yaani www.immigration.go.tz na kisha kwenda katika chaguo la e-services.

Hatua ya tatu mwombaji anapaswa kuchagua fomu ya ya maombi ya hati, kisha kuchagua ombi jipya, na kuweka tiki katika kiboksi ili kukubaliana na maelekezo yaliyotolewa.

Hatua ya nne mwombaji atatakiwa kujaza fomu inayomtaka kutoa taarifa zake binafsi mara baada ya kukamilisha kujaza fomu hiyo, atafahamishwa kuwa usajili wake umekamilika na kisha itatolewa namba ya ombi.

Ambapo inashauriwa ni lazima kuhifadhi namba hiyo kwa kuiandika pembeni kwa ajili ya kumbukumbu za baadae.

Kisha mwombaji atapewa namba ya kumbukumbu ya malipo na kutakiwa kwenda kulipia malipo ya awali ya sh 20,000.

Baada ya kukamilisha malipo ya awali mwombaji atatakiwa kufanya muamala wa pili kupitia simu yake katika menu ya tigo pesa au mpesa na kulipia bili na kisha kuingiza namba ya kampuni 888999.

Mara baada ya kumaliza kufanya mialama hiyo mwombaji atapa ujumbe kutoka kwenye mfumo namba 15200 kama muamala umekubalika kisha kurudi katika ombi au simu na namba ya risiti na kisha utapa maelekezo jinsi ya kupakua fomu yako.

Mara baada ya kupakua fomu muombaji atatakiwa kuiwasilsiha fomu hiyo katika ofisi za Uhamiaji makao makuu au ofisi kuu Zanzibar.

Malipo ya fedha kwa ajili ya hati mpya ya kusafiria yanaweza kufanyika kupitia benki NMB/CRDB mabapo mwombaji atapaswa kujaza fomu ya malipo ya kielektroniki, kufuata maelekezo kama yalivyotolewa.

Mara baada ya kukamilisha taratibu zote mwombaji anaweza kupata hati yake mpya ya kusafiria ndani ya muda wa wiki mbili ambayo ni sawa na siku 14 za kazi.

Burundi yapingana na takwimu za UNHCR
Mwigulu apinga kurundika vyuma chakavu