Kutokana na kuwepo kwa taaria za upungufu mkubwa wa chakula katika baadhi ya maeneo hapa nchini, Kiongozi wa Chama Cha  ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe,ameitaka Serikali kutangaza baa la njaa kutokana na ukubwa wa tatizo hilo nchini.

Aidha, amesema kuwa tamko la baa la njaa litaisaidia Serikali kupata bajeti ya dharula ya kununua chakula na kutoa kwa wakuu wa wilaya kutangaza bila woga kuwa maeneo yao yana njaa.

“Nampongeza sana Waziri Mkuu Majaliwa kwa kuamua yeye mwenyewe kutembelea ghala la chakula la NFRA na kujionea hali halisi,Huu ndio uongozi badala ya kukanusha habari ambazo ni za kweli kabisa na kudhibitishwa na taasisi za serikali kama Benki kuu ya Tanzania,”amesema Zitto.

Zitto amesema kuwa baada ya Waziri Mkuu kujionea tatizo hilo,,anapaswa kuchukua hatua dhidi ya viongozi wa serikali wanaoficha ukweli kuhusu baa la njaa inchini.

Hata hivyo, Zitto amesema kuwa takwimu za kiasi cha chakula ziko kwenye tvuti ya Benki ya Tanzania, Waziri wa kilimo alikuwa anajaribu kuficha kwa kuogopa kutumbuliwa kwa kusema hali halisi ya chakula nchini.

Belle 9: Diamond ni mdogo wangu siwezi kumuiga kwa chochote
Lowassa, Maalim Seif kufuta nyayo za Kinana Zanzibar Kesho?