Mbunge wa Kigoma Mjini ambaye ni kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe ameelezea kushangazwa na hatua ya serikali inayotumbua majipu kulilea jipu linaloiingizia taifa hasara ya shilingi bilioni 4 kila mwezi.

Zitto amekosoa hatua ya serikali kuufumbia macho ufisadi unaoendelea kufanywa kwa kumlipa Harbinder Singh Seth ambaye ni mmiliki wa kampuni ya IPTL shilingi bilioni 4 kila mwezi kama gharama za kuiuzia Umeme Tanesco.

Serikali ya awamu ya tano imeshailipa IPTL malipo ya miezi miwili ambayo ni shilingi bilioni 8.

Zitto ameyasema hayo baada ya serikali kutoa tangazo kuhusu kashfa ya Commodity Import Support ya miaka 1980s na 1990s. Amehoji kwanini serikali imeendelea kuing’ang’ania kashfa hiyo pekee na kuacha kuchukua hatua dhidi ya ufisadi wa IPTL unaoligharimu taifa kiasi kikubwa cha fedha kila mwezi.

Mahakama Yaweka Zuio la Muda Bomoabomoa, Ni kwa Nyumba Hizi Pekee
Azam FC Yakamatwa Na Yanga Zanzibar, Ubabe Watawala