Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia Chama Cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa serikali imeshindwa kupeleka trilioni 1 benki kuu ya Tanzania (BoT) zinazo hitajika kwenye akaunti maalumu.

Ameyasema hayo jijini Dodoma wakati akichangia hoja katika mjadala wa ukuzaji wa viwanda katika sekta ya madini na uzinduaji katika wiki ya asasi za kiraia.

Amesema kuwa tatizo ni kutokutekelezwa kwa sheria zinazotungwa na bunge na kwamba mwaka 2015, Bunge lilitunga sheria ya kusimamia fedha za mapato ya gesi na mafuta.

“Mapato yote yanayo kusanywa na shirika la TPDC na kodi ya mapato inayokusanywa na TRA yanaelekezwa na sheria kwenda kwenye akaunti maalumu Benki Kuu inaitwa Revenue Holding account, sheria hiyo (Oil and Gas Revenue Management Act. No 22 ya 2015) kifungu cha 8 inaanzisha mfuko huo maalumu,”amesema Zitto

Aidha, amesema kuwa zaidi ya shilingi trilioni 1. 29 hazija kwenda kwenye mfuko na zinatumika bila kufuata utaratibu kama sheria inavyoelekeza.

Kwa upande wake meneja msaidizi wa idara ulipaji kodi kimataifa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Alfredy Mkinga amesema kuwa sheria inayosimamia mapato yanayotokana na rasilimali hizo inalenga kuwezesha vizazi vijavyo.

Fahamu mji hatari kwa maisha ya wanawake
Robin van Persie kustaafu soka