Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amempa sifa zaidi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli kwa kufanya kazi iliyowashinda viongozi wa nchi nyingi kubwa duniani.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amesema kuwa Magufuli ameweza kuondoa fikra iliyowapa kinga baadhi ya vigogo na watu wazito ambao huwa na kinga ya kutoguswa hata wanapokosea.

“Jambo kubwa la msingi Rais Magufuli analifanya kwa sasa nchini ni kuondoa ‘kutogusika’ kwa kimombo IMPUNITY. Kwamba unaweza kufanya jambo na usiwajibishwe kwa jambo hilo. Impunity ni moja ya kiini cha ufisadi kwenye nchi nyingi zinazoendelea. Rais ameonyesh dhamira ya dhati katika eneo hilo na ni muhimu aungwe mkono. Levels of impunity were too high,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Polisi yawatupa gerezani ombaomba 17, yawashikilia wengine
Jenerali wa Jeshi la Burundi na Mkewe wauawa