Siku moja baada ya baadhi ya mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano kusukumwa na Rais John Magufuli kuwasilisha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Tamko la Rasilimali, Maslahi Madeni pamoja na Uadilifu, Zitto Kabwe ameshindilia msumari.

Mbunge huyo wa Kigoma Mjini ametaka Rais John Magufuli kutoa amri kwa Sekretarieti hiyo kuweka mtandaoni fomu za mali na madeni ya viongozi hao ili kila mtu aweze kuziona.

“Rais Magufuli aagize Mali na Madeni ya Viongozi yawekwe wazi kweny tovuti ya Tume ya Maadili ya Viongozi ( sheria irekebishwe kuzuia watu wanaoona matamko kuziweka wazi, bila uwazi ni vigumu kupambana na rushwa),” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Zitto ambaye ni Kiongozi Mkuu wa ACT – Wazalendo, amekuwa akisisitiza kuwa chama chake kimeweka msimamo wa kuhakikisha Maadili yanazingatiwa na viongozi na kwamba katiba ya chama hicho inamtaka kila kiongozi kutangaza mali na madeni yake.

CUF kuandamana kupinga uchaguzi wa Marudio Zanzibar
Shabiki amtega Ali Kiba... Ni kama alitaka aangukie kwa Diamond