Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Ruyagwa Kabwe amemshauri Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai kuwa na msimamo katika kuisimamia serikali kama alivyofanya jana pindi alimpomtaka Waziri Mwijage kutoa majibu ya kuridhisha juu ya sakata la sukari na mafuta.

Zitto Kabwe amesema hayo baada ya jana Mei 8, 2018 Spika wa Bunge kumtaka Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage kuja na maelezo ya kutosha kuhusu tatizo la sukari na mafuta nchini baada ya kutoridhishwa na majibu ya waziri huyo bungeni na kusisitiza kuwa haiwezekani wananchi wakawa wanaumia kwa gharama kubwa ya bidhaa hizo.

“Namna ambavyo Spika Ndugai amesimamia suala la majibu ya Serikali kuhusu kadhia ya Sukari na Mafuta ya Uto (kula) inanikumbusha bunge la tisa. Ndugai sasa ameanza kuweka ‘legacy’ yake. Aendelee hivi hivi ila jambo la muhimu zaidi suala la mafuta litazamwe kwa muktadha wa Wakulima wa Mawese na Alizeti” alisisitiza Zitto Kabwe

Kutokana na Spika wa Bunge na bunge kiujumla kutoridhika na majibu ya Waziri Mwijage hivyo spika wa bunge Job Ndugai aliomba maelezo zaidi na kutaka swali hilo kuulizwa tena wiki ijayo ili serikali ije na majibu ya kueleweka na yenye tija.

Jinsi ya kuishi na Bosi anayekupa ‘stress’
Kessy awalipua viongozi na watoto wa vigogo Bungeni