Mbunge wa Kigoma Mjini na Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amefunguka na kuwataka Wabunge wa vyama vya upinzani wasimame mbele ili waweze kuhesabiwa ili wapate kujitambua wamebakia wangapi.

Zitto amebainisha hayo kupitia ukurasa wake maalumu wa kijamii baada ya kutolewa kwa hukumu ya Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga kwenda jela miezi mitano kutokana na kukutwa na hatia ya kutoa maneno ya kashfa dhidi ya Rais Magufuli.

“Nimeona mashtaka ya Sugu yaliyopelekea kuhukumiwa kwenda jela miezi 5” amesema Zitto

Pia Zitto ameachiwa huru siku chache zilizopita baada ya kukamatwa na Jeshi la polisi mkoani Morogoro kwa kufanya mikutano ya hadhara bila kibali maalumu, Mbunge huyo ambaye aliachiwa kwa dhamana ya milioni 5O, na kudai kuwa ataendelea na Ziara yake kama alivyokusudia.

Aidha Zitto amelalama kuwa kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kuwasweka jela upinzani wote au kutorudia kufanya walichomfanyia Sugu.

Wabunge wote wa vyama vya upinzani kwa namna moja ama nyingine tunasema haya kila wakati kwenye mikutano yetu. Kuna haja ya kufanya jambo ambalo dola itaamua kutusweka jela wote au kutorudia walichofanya kwa Sugu”, amesema Zitto.

Wanafunzi 111 wapotea baada ya shambulio la Boko Haramu
Kibatala kukata rufaa, Wasanii wafunguka hukumu ya Sugu