Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka marais wastaafu kutokaa kimya, badala yake wajitokeze kumshauri rais Magufuli wanapoona mambo hayaendi sawa ili kunusuru nchi na uchumi.

Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya Isagehe, Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

“Hii nchi inaongozwa kwa misingi ya kidemokrasia, nawaomba marais wastaafu wasikae kimya kuhusu kunusuru nchi, wamshauri rais kuhusu mambo mbalimbali likiwemo la vyama vya siasa kuzuiwa kufanya mikutano ya hadhara,”amesema Zitto.

Aidha, Zitto amemuomba rais Magufuli kufanya mabadiliko katika sekta ya madini kwa kuweka wazi mikataba ya wawekezaji na kwamba jambo hilo litasaidia wananchi kuwa na uelewa wa mikataba hiyo.

Hata hivyo, Zitto ameshangazwa kuona barabara inayounganisha migodi mitatu ya  dhahabu ya Buzwagi, Bulyanhulu na Geita Gold Mine kuwa barabara hiyo haina kiwango cha lami.

Masele: kwa heri ukapera
Allegri Ajibu Tetesi Za Kumrithi Arsene Wenger