Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amedai kuwa makosa anayoshtakiwa yanafanana na makosa ambayo walishawahi kushtakiwa baadhi ya waasisi wa bara la Afrika.

Amesema kuwa kesi za namna hiyo ndizo zilizowahi kuwakumba baadhi ya waasisi, akiwemo muasisi wa Taifa la Afrika Kusini, Nelson Mandela pamoja na muasisi wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.

“Kesi za namna hii wamefungwa wakina Mandela, na mwalimu kwa hiyo sio jambo linapaswa kuwatisha watu. Ila nasikitika sana jana sikushiriki kongamano la chuo kikuu cha Dar es salaam.”amesema Zitto

Aidha, mbunge huyo wa Kigoma Mjini anashtakiwa kwa makosa matatu ya uchochezi, ambapo katika kesi yake upande wa Jamhuri unawakilishwa na Wakili, Tumaini Kweka na upande mshtakiwa unawakilishwa na wakili Peter Kibatala.

Hata hivyo, Zitto alikamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam oktoba 31 mwaka huu kufuatia mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alitoa madai ya kuuawa kwa zaidi ya raia 100 katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma, taarifa ambayo ni tofauti na ile ya Jeshi la Polisi mkoani humo.

Kesi ya Mbunge huyo inatarajiwa kuendelea tena novemba 12 mwaka huu

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Novemba 3, 2018
Unafikiria Kubadili Kazi? Ishara 6 za Kuzingatia