Kiongozi Mkuu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe anaendelea kushikilia msimamo wake juu ya mgogoro wa kisiasa unaendelea visiwani Zanzibar kufuatia tangazo la kufutwa kwa Uchaguzi.

Zitto ameitaka ZEC kumtangaza mshindi wa uchaguzi huo kwa kuwa uchaguzi ulishafanyika na kwamba ulienda vizuri kwa mujibu wa watazamaji wa ndani na nje.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini alisema kuwa ZEC wanapaswa kutumia busara na kumtangaza Maalim Seif Sharif Hamad ili kuepusha shari.

“Wangefanya mapema tu, wamtangaze Maalim Seif aunde serikali. Wakifanya hivyo hawatapoteza chochote maana kwa mujibu wa Katiba ya Zanzibar, (CCM) wataendelea kuwa ndani ya serikali, “Zitto aliiambia Mwananchi.

Zitto aliendelea kusisitiza kuwa hakuna namna ambayo itaiwezesha CCM kushinda Zanzibar hata kama uchaguzi huo utarudiwa.

Alisema kuwa chama cha wananchi CUF kimeoneosha dalili zote za kushinda uchaguzi huo ikiwa ni pamoja na kuvunja ngome ya CCM upande wa Unguja na kushinda viti 9 tofauti na zamani  ambapo ilikuwa ikishinda viti viwili tu.

“CCM walikuwa na madiwani Pemba lakini sasa hivi hawana hata mmoja. Yaani hakuna jinsi watashinda Zanzibar. Wanachofanya ni kujidanganya mpaka watakapogundua hawana nguvu tena ndipo wataachia madaraka,” alisema.

 

 

Makontena Tisa Yakamatwa Dar
Miss Tanzania Akumbwa Na Kashfa Ya Ufisadi Wa Shilingi Trilioni 1.3