Kitendo cha Mbunge wa Arusha mjini kukaa rumande kwa zaidi ya miezi minne sasa pasipo kupatiwa dhamana kimemfanya Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kushindwa kuzuia hisia zake na kutaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali iwajibishwe

Zitto amedai kuwa kitendo cha  Mbunge huyo ambaye ni mwakilishi wa wananchi kunyimwa dhamana  ni siasa za ukomoaji ambazo zinajenga chuki kwenye jamii ambapo chuki huwa zinazaa visasi.

“Haitoshi Majaji kukemea Ofisi ya DPP, Mfumo wetu lazima uweke uwezo wa waendesha mashtaka wa aina ya kesi ya Mbunge wa Arusha Mjini kuwajibishwa. Wanasheria tazameni namna ya kuwajibisha Ofisi ya DPP kwa uonevu wa makusudi dhidi ya wananchi,” amesema  Zitto.

Hata hivyo kauli hiyo ya Zitto imekuja baada ya  majaji watatu  kutoka mahakama ya rufaa kuitaka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali na DPP kuwa makini na kuwataka kuwashikilia watu kwa misingi ya kisheria na kuongeza kuwa haipendezi na haingii akilini mtu  kushikiliwa kwa miezi minne bila sababu kwa misingi ya kumnyima haki ya dhamana.

Makonda apigwa changa la macho eneo la Kigamboni
Video: 'Wanaomiliki ardhi mjini bila hati kutozwa kodi' - Lukuvi