Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe leo anatarajiwa kuanza kujitetea Mahakamani kufuatia kesi dhidi yake pamoja na Gazeti la Raia Mwema iliyofunguliwa na mmiliki wa kampuni ya IPTL, Harbinder Singh Seth.

Harbinder Seth

Harbinder Seth

Mmiliki huyo wa IPTL iliyohusishwa na sakata zito la uchotwaji wa fedha kwenye akaunti maalum ya Tegeta Escrow iliyokuwa imefunguliwa kwa lengo la kuhifadhi fedha kusubiri utatuzi wa mgogoro kati ya IPTL na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), anawatuhumu Zitto na Mhariri wa Raia Mwema kwa chapisho analodai lina habari ya uongo inayolichafua kampuni hiyo pamoja na mmiliki wake.

Seth anadai fidia ya shilingi bilioni 500 kutokana na athari alizopataka kwa chapisho hilo lililomhoji Zitto Kabwe.

“Kesi ya IPTL/PAP/Harbinder Singh dhidi ya Zitto Z Kabwe na RaiaMwema leo mbele ya Jaji Bongole. Wanataka fidia ya tshs 500bn kwa kuchafuliwa jina!,” Zitto ameandika kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Hivi karibuni, mmiliki wa IPTL alimtuhumu Zitto Kabwe kwa kuongoza uchunguzi wa Sakata la Escrow Bungeni na kuwasilisha mapendekezo wakati alikuwa na maslahi kwenye sakata hilo. Alisema wakati Zitto akiwa Mwenyekiti wa PAC, alikuwa tayari na kesi dhidi ya mmiliki wa IPTL hivyo alipaswa kutangaza hadharani na kujitoa kwenye uchunguzi wa sakata hilo lililoihusisha IPTL lililosababisha mawaziri kadhaa kuondolewa.

Anne Malecela aeleza sababu za ‘kulikuna’ jicho la Magufuli
Baada Ya Ushindi Wa Tatu Bila, Stewart Hall Aahidi Mazito