Mbunge wa kigoma mjini, Zitto Kabwe ambaye pia ni kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo, amevunja ukimya akisema  mwaka 2016 ulikuwa wa kupambana na ufisadi.

Aidha, Zitto ameipongeza Serikali katika vita dhidi ya ufisadi  ambao ulikuwa sehemu ya maisha ya watu tofauti na sasa ambapo ufisadi umekuwa gharama hivyo umepungua kwa kiasi kikubwa.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa udiwani kwenye kata ya kijichi, Manispaa ya Temeke ambapo chama hicho kimesimamisha mgombea, Edgar Mkosamali.

“Tunasisitiza Rais aone jema hili kwani atakuwa anarejesha Tanzania ya Mwalimu Nyerere, kwani miiko ya uongozi ilikuwa nguzo kuu ya siasa ya Azimio la Arusha la Chama cha TANU, sisi ACT tulihuisha Azimio la Arusha  kwa kutangaza Azimio la Tabora”amesema Zitto

Aidha, Zitto amesema kuwa mwezi Februari mwaka huu wataadhimisha miaka 50 ya Azimio la Arusha kwa kufanya Mkutano Mkuu  wa kidemokrasia jijini Arusha.

 

Mourinho: Sijafurahishwa na kuondoka kwa Erick Bailey
Serikali kulipa madeni yote ya Maliasili