Kiongozi Mkuu wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe ameendelea kuwatetea wanasiasa wakongwe wa upinzani waliengua katika harakati za kumsapoti mgombea wa vyama vya upinzani vinavyounda Ukawa, Edward Lowassa.

Akionesha kuunga mkono uamuzi wa wanasiasa hao, Zitto Kabwe ametumia akaunti yake ya Twitter kuwatahadharisha wananchi kuwa watawakumbuka baada ya uchaguzi mkuu kumalizika, Oktoba 25 mwaka huu.

“Watu ambao walipigania mabadiliko nchi hii ni Lipumba na Dr Slaa leo hii hawapo kwenye siasa kwa hiyo tusitegemee katiba mpya,” aliandika Zitto.

“Leo wameondoka ila baada ya uchaguzi mkuu tutawakumbuka hawa akina Lipumba na Dk Slaa,” aliongeza.

Katika hatua nyingine, Zitto alikosoa ahadi ya mgombea wa CCM, Dk John Magufuli ya kuwanyang’anya wawekezaji mashamba wasiyoyaendeleza huku akidai kuwa mgombea huyo aliipinga hoja hiyo bungeni mwaka 2011 ambapo Zitto alitaka serikali kuchukua mashamba ya mkonge.

“Mwaka 2011 nilipeleka hoja binafsi kurudisha mashamba ya katani kwa wananchi na alikuwa bungeni alipinga leo hii analeta mpya gani?”

Kiongozi Mkuu huyo wa ACT – Wazalendo alieleza kuwa mgombea pekee anaeweza kuleta mabadiliko ya kweli ni mgombea urais kupitia chama hicho, Bi. Anna Mghwira.

Lowassa Aeleza Atakapotoa Fedha Za Kutekeleza Ahadi Zake
Aunt Ezekiel Aihama Ukawa? Mwenendo Wake Unaongea