Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini,  Zitto Kabwe amesema kuwa kauli iliyotolewa na serikali ikiwashutumu vyama vya upinzani kushiriki na kutoa taarifa za ndege kuzuiliwa nchini Canada sio ya haki kwani wananchi wanapaswa kujua kila kitu kinachoendelea kuhusu nchi yao.

Amesema kuwa suala kama hilo ni lazima watu wahoji, na sio kama hawapendi maendeleo yanayofanywa na uongozi wa Rais Dkt. Magufuli, isipokuwa wanataka serikali ifanye vitu kwa uhakika zaidi, ili kuepusha kujiingiza kwenye hasara na migogoro kama hiyo.

“hatukutaka mnunue ndege hovyo hovyo, lakini ndege tunataka na tunapanda, mkihojiwa mnaleta viroja, jibuni hoja tu viroja vya nini, Watu ni lazima wahoji mtake mistake, hakuna anayetaka msubiri, tunataka mfanye kwa  uhakika, tutaendelea kuhoji na lazima  serikali ijibu,”amesema Zitto kwenye ukurasa wake wa Twitter

Aidha, tar 18 Agosti mwaka huu mbunge wa Singida Mashariki na mwanasheria mkuu wa (CHADEMA), Tundu Anthipas Lissu, alitoa taarifa kuwa kuna mali za Tanzania zimezuiliwa nchini Canada kutokana na deni ambalo serikali inadaiwa na kampuni ya ukandarasi.

Hata hivyo, siku moja baada ya taarifa hizo kutolewa, serikali kupitia kwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zamaradi Kawawa ilithibitisha uwepo wa suala hilo na kuongeza kuwa kuna baadhi ya watu  wa vyama vya upinzani wameshirikiana na makampuni ya nje kufungua kesi kama hizo.

Video: Aliyetumbuliwa arejeshwa kazini
Msimamizi wa uchaguzi akutwa ameuawa nchini Kenya