Kiongozi mkuu wa chama cha ACT- Maendeleo amewapima wagombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na Mgombea wa Chadema ambaye atabeba bendera ya Ukawa, Edward Lowassa na kudai kuwa hawezi kupambana na ufisadi.

Zitto ameyasema hayo hivi karibuni wakati anawahutubia wananchi katika katika jimbo la Kigoma mjini uliohusu mchakato wa kura za maoni kumpata mgombea ubunge wa chama hicho.

Zitto aliongeza kuwa chama chake kina upekee wa sera na msimamo ambao vyama vingine vya upinzani havina, hususan kanuni na taratibu za maadili ya uongozi.

Alisema uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa kihistoria ambao utatoa picha tofauti ambayo haitakiruhusu chama kimoja pekee kuunda serikali yake kutokana na ushindani mkubwa uliopo.

“Uchaguzi wa mwaka huu hata kama chama kimojawapo kitashinda hakiwezi kuunda serikali peke yake na kama kuna jambo ambalo tutalifanya wapinzani na wananchi wasitusamehe ni kushirikiana na CCM,” alisema Zitto Kabwe.

Mwanasiasa huyo ambaye alitengeneza jina kubwa zaidi alipokuwa katika Chadema, alisisitiza kuwa ni ACT-Maendeleo pekee kwa sasa ambayo ina uwezo wa kutekeleza sera zake kwa kupambana na ufisadi nchini.

Ferguson Amshukuru Rooney
Diego Costa Kuwakosa Swansea City