Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amezungumzia hali ya siasa nchini ambapo amesema hali imebadilika sana kwababu Serikali mpya ina namna yake ya utendaji hivyo ni dhahili kwamba siasa iko tofauti.

Zitto amesema ajenda zimebadilika kwa sasa kwani awamu ya nne ajenda kuu upande wa vyama vya upinzani ilikuwa ni ufisadi tofauti na sasa kwani Serikali yenyewe chini ya kiongozi wa nchi Rais John Pombe Magufuli inashughulikia ufisadi yenyewe, kwahiyo vyama vya Upinzani pamoja na kuendelea kusimamia Serikali lazima kuangalia ni maeneo yapi Serikali haiendi sawa.

Amesema sasa hivi mkuu wa nchi Rais Magufuli analipua mabomu mwenyewe hali inayowafanya Mawaziri wake kukimbizana na spidi yake huku na kule  ili waonekane wanafanya kazi.

Zitto amesema sasa hivi utaonekana ni mwanasiasa mahili kutokana na utekelezaji zaidi, na namna gani umejibu changamoto za wananchi unaowaongoza tofauti na takribani miaka 10 iliyopita kwamba ni kwa namna gani ambavyo unaibua uozo katika utendaji wa Serikali.

Akizungumzia hali ya Ukawa amesema kuwepo kwa umoja huo kabla na baada ya uchaguzi ni hatua kubwa sana na yakupongezwa mbali na kwamba kunaweza kukawa na madhaifu ndani ya umoja huo lakini madhaifu hayo hayaondoi ukweli kwamba ni hatua kubwa sana katika mfumo wetu wa siasa.

Waziri Nchemba aagiza msako wa walimu wanaoonekana kwenye video wakimshambulia mwanafunzi
Video: Mzee Chilo ndani ya 'Mtoto mdogo' ya Shilole