Baada ya Kampuni ya uchimbaji madini nchini, Accacia kusema kuwa haina fedha za kuilipa Serikali ya Tanzania kama ilivyodaiwa na Barrick Gold Mine, Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amesema kuwa serikali ilikosea kutangaza ushindi mapema.

Zitto amesema kuwa alitegemea kauli kama hiyo kutoka kwenye Kampuni ya Accacia kwani siyo mara ya kwanza kwa Kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama hiyo kwani hata miaka ya nyuma walipobanwa na bunge kuhusu suala la misamaha ya kodi walifanya hivyo.

Aidha, amesema kuwa alishangaa sana kusikia serikali ikisema kuwa imefanikiwa kwani haikuwa ikizungumza na kampuni ya Accacia bali mmiliki wa kampuni ya Barrick na kutokana na sheria ya Makampuni Mmiliki kama mmiliki anasimama mwenyewe na kampuni husimama yenyewe.

“Nilitegemea hili kutokea baada ya serikali kutangaza hayo, Ni makosa tuliyoyafanya wenyewe. Serikali kutangaza ushindi kwenye mazungumzo waliyofanya na kampuni hiyo yalikuwa ni makosa kwani ni kawaida kwa kampuni ya Barrick kutoa ahadi kama waliyokuwa wameitoa na walishafanya hivyo kwa nchi ya Bolivia, na Chille. Serikali inapaswa sasa irudi kukaa mezani na Accacia wenyewe kwa ajili ya mazungumzo,”amesema Zitto

Hata hivyo, Kampuni ya uchimbaji madini, Acacia (Acacia Mining) imesema kuwa haina uwezo wa kulipa dola milioni 300 kwa serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili kutatua mgogoro wa kodi.

Serikali ya Hispania kutangaza hatua dhidi ya jimbo la Catalonia
Umoja wa Ulaya wazidi kuvutana kuhusu Uingereza