Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa wamekubaliana na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe kuungana kwa heshima ya marehemu Bilago kugombea ubunge jimbo la Buyungu.

Ambapo kwa pamoja wataangalia mgombea mwenye ushawishi zaidi katika jimbo hilo iwe kutoka ACT Wazalendo au Chadema na kumuweka kuwa mgombea rasmi wa ubunge wa jimbo hilo.

“Kwa heshima ya Mwalimu Bilago Mimi na Freeman Aikaeli Mbowe tumekubaliana kuwa tutashawishi kuwepo na Democratic Front Katika Jimbo la Buyungu.

Ambapo amasema ACT Wazalendo watamuunga mkono mgombea wa Chadema au Chadema watamuunga mkono mgombea wa ACT Wazalendo.

“Tunataka kuweka mgombea mmoja anayekubalika na wananchi wa Buyungu na kufanya kampeni kwa pamoja mpaka ushindi.“amesema Zitto Kabwe.

“Huu ni mwanzo wa harakati za kuwa na United Democratic Front dhidi ya ukandamizaji wa Demokrasia nchini na dhidi ya Hali mbaya ya Maisha ya Watu wetu. Umoja wa zaidi ya vyama vya siasa ukihusisha Vyama vya Wafanyakazi, Vyama vya Wakulima, Vyama vya Wafanyabiashara na Wananchi wengine.“amemaliza Zitto.

Jimbo la Buyungu kwa sasa lipo wazi baada ya aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo kupitia tiketi ya CHADEMA, Kasuku Samson Bilago kufariki dunia mnamo Mei 25, 2018 .

Makonda atoboa siri, ndoa ya Majizo na Lulu
Ngasa arejea nyumbani 'Yanga'