Mbunge wa Kigoma na Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe ametoa matamko yake akidai kuwa anamuomba Mwenyezi Mungu ampe uhai na nafasi ya kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa siku zijazo, akiamini kuwa ipo siku itakuwa hivyo kwani hakuna aijuaye kesho yake.

“Namuomba sana Mungu ampe uhai Job Ndugai na pia anipe uhai na kama kuna kheri ndani yake anipe nafasi ya kusaidiana na wenzangu kuongoza nchi yetu, hakuna ajuaye ya kesho isipokuwa Mungu tu”.

Zitto ametoa dua hiyo akimjibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai aliyezungumza mbele ya Bunge kuwa Zitto Kabwe hawezi kuwa Rais wa nchi akidai kuwa jambo hilo haliwezekani.

Ndugai hakutoa maelezo ya kutosha juu ya kauli hiyo, ila aliongea hayo mara baada ya Waziri wa zamani wa TAMISEMI, George Simbachawene wakati akichangia mada juu ya Muswada wa Vyama vya Siasa na kumtolea mfano Zitto Kabwe kuwa ni Rais wa nchi na kuhoji kuwa itakuwaje akishuhudia wapinzani wakiendesha shughuli za maandamano.

”Mheshimiwa Simbachawene bahati nzuri Zitto hawezi kuwa Rais wa nchi haiwezekani.” Amesema Ndugai.

Zitto hakuifumbia macho kauli hiyo ya Spika Job, kupitia ukurasa wake wa Twitter aliamua kufunguka na kumuomba Mungu ampe uhai Job Ndugai, lakini pia ampe uhai yeye ili aweze kumshuhudia akiongoza nchi.

 

 

Mchungaji mbaroni kwa kuuza tiketi za kwenda mbinguni
Lema ajitosa sakata la Lissu, 'niko tayari kujiuzulu'

Comments

comments