Mbunge wa Kigoma Mjini kupitia ACT-Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amesema kuwa mwaka 2017 ulimgharimu baada ya tukio la kupigwa risasi Tundu Lissu.
 
Katika ukurasa wake wa facebook, Zitto Kabwe amesema kupigwa risasi kwa Tundu Lissu kulimfanya abadili mtazamo wake na kumfanya kupoteza watu wa karibu.
 
“Tukio la kupigwa risasi Mbunge Tundu Lissu ni tukio baya sana na lilibadilisha kabisa mtazamo wangu wa mapambano ya kulinda Demokrasia. Ilinigarimu kwa kupoteza watu wa karibu kufuatia kuwa mkali sana kulaani tukio lile. Sijutii kwani niliamini kuwa lengo la waliotaka kumwua Lissu lilikuwa kutunyamazisha na hivyo majibu sahihi yakawa ni kusema zaidi”, ameandika Zitto Kabwe
 
Hata hivyo, Zitto ameongeza kuwa tukio lingine alilokumbana nalo 2017 ni kitendo cha kuondoka kwa wanachama waandamizi na kuhamia chama kingine, huku akilielezea kuwa limekuwa funzo kubwa kwake.
  • Polepole: Hakuna kiongozi anayetishiwa
  • Mke wa Kafulila amtembelea Lissu
  • Mbowe: Futeni vyama vingi kama havina umuhimu

JPM awatakia kheri ya mwaka mpya Watanzania
Video: Mimi ni tajiri wa dunia- Kakobe