Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, amesema anazo taarifa juu ya wapi alipo kijana Raphael Ongangi ambaye ni raia wa Kenya aliyetekwa Juni 24, 2019, na watu wasiojulikana jijini Dar es salaam wakati akitoka shuleni kwa watoto wake kwenye kikao cha wazazi.

Zitto ametoa rai kwa watekaji kwamba wamuachie Raphael kwani hana taarifa zake zozote na aliacha kufanya naye kazi miaka mitatu iliyopita na kudai kuwa, masuala ya utekaji ni ushamba hivyo wamuachie akajiunge na familia yake.

”Tuwaombe tu watekaji wamuachie maana hana taarifa zozote, na kosa kubwa walilolifanya watekaji ni kuanza kuutumia ukurasa wangu kuandika mambo yanayomsifia Magufuli, hiyo inamaana kwamba wanaomuunga mkono Magufuli ndiyo watekaji”, amesema.

Zitto ameongeza kuwa, wao kama marafiki wa Raphael wamefanikiwa kupata hadi mahali alikowekwa baada ya kutekwa, na baadhi ya taarifa wamewapa polisi na kwamba wanajua walipomuweka kuanzia siku ya kwanza hadi Jumamosi.

”Niwaombe watekaji wasifanye mambo yoyote ya kijinga kwani gharama yake ni kubwa, wamuache kokote sisi tutaenda kumchukua”.

Zitto amesema masuala ya utekaji hayaleti  taswira nzuri kwa nchi na  nchi jirani, na kwamba  vyombo vya usalama vya Taifa vimekuwa vikihusishwa na masuala haya kitu ambacho ni aibu, na hivyo ni vyema watoke wajisafishe kwa jamii na kwamba itafikia hatua watekaji na wao wataanza kutekwa.

Aidha, Zitto Kabwe ameitaka Serikali ya Tanzania kufuatilia kwa uzito tukio la kutekwa kwa aliyekuwa msimamizi wake, Raphael Ongagi ambaye.

Mfungwa ajiua mbele ya mkuu wa gereza
CEO wa Safaricom afariki dunia

Comments

comments