Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amesema yeye ni kiongozi tofauti na wanachama wengine hivyo hakuna uteuzi utakaofanyika kwake bila mamlaka ya uteuzi na chama kufanya majadiliano 

Kwa mujibu wa East Africa Radio katika kipindi cha Supa Breakfast, amesema kuwa endapo atateuliwa atakubali au la, ambapo kiongozi huyu amesema uteuzi wa kiongozi wa chama cha siasa utahitaji majadiliano kwani unaweza ibua taharuki.

“Hakuna uteuzi wowote utakaofanywa kwa Zitto utakao kuwa wa halali bila majadiliano kati ya mamlaka ya uteuzi na chama, na ni kwa ajili ya nini, kwa shughuli zipi kwa makubaliano yapi, kuteuliwa kwa mtu yeyote ni sawa ila mimi ni ni kiongozi wa chama,” amesema Zitto

Aidha Zitto ameongeza kuwa “Tangu mwanzo tunasema nchi yetu inahitaji Katiba mpya, na ni takwa la Watanzania, msimamo wetu upo wazi lazima nchi irudi kwenye mjadala wa Katiba mpya na lazima iwe matokeo ya mazungumzo na viongozi wa kisiasa na sio mashinikizo,”

Zitto amesema katika uchaguzi uliofanyika katika majimbo la Buhigwe na Muhambwe waliwasilisha barua yao kwa mamlaka husika kuelezea changamoto zilizopo ambazo haziwezi kutatuliwa bila kuwa na tume huru ya uchaguzi huku akitaraji suala hili kuwa moja ya kipengele cha majadiliano siku viongozi wa vyama vya siasa watapokutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Wazee waomba ulinzi kwa Rais Samia dhidi ya ukatili
Samia aagiza viwanja vya mchezo kurekebishwa