Aliyekua nahodha na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Sweden Zlatan Ibrahimovic amefikisha mabao 500, tangu alipoanza kucheza soka mwaka 1999 akiwa na klabu ya Malmö FF.

Zlatan alifikisha bao la 500 katika mchezo wa ligi ya nchini Marekani ulioshuhudia klabu yake ya La Galaxy ikiibuka na ushindi wa mabao matano kwa matatu dhidi ya Toronto jana jumapili, kwenye ligi ya nchini Marekani (MLS).

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 36, alifunga bao moja miongoni mwa mabao matano yaliyowapa ushindi katika mchezo huo, ambao ulishuhudiwa na mashabiki wengi nchini Marekani.

Kwa hatua hiyo Zlatan anajiunga na washambuliaji Cristiano Ronaldo na Lionel Messi, ambao tayari wameshafunga mabao 500 na zaidi tangu walipoanza kutambuliwa katika medani ya soka duniani.

Tangu alipotua katika ligi ya nchini Marekani (MLS) Zlatan ameshafunga mabao 17 katika michezo 22 aliyocheza.

Bado anatarajiwa kuendelea kufunga mabao katika ligi ya nchini Marakeni, kutokana na umahiri na uwezo ambao amekua akiuonyesha, jambo ambalo linaendelea kumpa faraja, licha ya kuwa na umri wa miaka 36.

Zlatan alijiunga na La Galaxy akitokea nchini England alipokua akiitumikia klabu ya Man Utd, ambayo alifanikiwa kuifungia mabao 17 katika michezo 33 aliyocheza.

Historia ya Zlatan tangu mwaka 1999.

1999–2001  Malmö FF michezo 40 mabao 16,  Ajax (2001–2004) michezo 74 mabao 35, Juventus FC (2004–2006) Michezo  70 mabao 23, Inter Milan (2006–2009) Michezo 88 mabao 57, FC Barcelona (2009–2011) Michezo 29 mabao 16, AC Milan (2010–2012) Michezo 61 mabao 42, Paris Saint-Germain (2012–2016) Michezo 122 Mabao 113, Manchester United (2016–2018) Michezo 33 Mabao 17 na LA Galaxy (2018–) Michezo 22  Mabao 17.

Timu ya taifa ya Sweden chini ya umri wa miaka 18 mwaka 1999 Michezo 4 bao moja, (2001) chini ya umri wa miaka 21, Michezo 7 Mabao 6, (2001–2016) timu ya taifa ya wakubwa, michezo 116 mabao 62.

Meddie Kagere awabwaga Mahundi, Mponda
Gabriel Zakuani awapisha vijana DR Congo