Uongozi wa klabu ya Società Sportiva Calcio Napoli, umethibitisha kuingia kwenye mbio za kumuwania mshambuliaji kutoka nchini Sweden, Zlatan Ibrahimovic, ambaye kwa sasa yupo huru baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia klabu ya PSG ya nchini Ufaransa.

SSC Napoli wamejiinga katika mbio hizo, kutokana na mipango waliyonayo kwa kwa sasa ya kutaka kumuuza mshambuliaji wao kutoka nchini Argentina Gonzalo Higuain.

Inaamiwa kwamba mbadala wa Higuain, ni Ibrahimovic ambaye kwa sasa yupo katika mikakati ya kusaka pahala pa kuendeleza soka lake.

Hata hivyo mpaka sasa bado haijafahamika kama mazungumzo kati ya viongozi wa SSC Napoli na wakala wa mshambuaji huyo kama yameshaanza, lakini tayari uthibitisho wa kuwa katika harakati za kumsajili umeshatangazwa.

Zlatan, amekua katika mipango ya kucheza soka popote pale atapata ofa nzuri, lakini aliwahi kusikika akisema kwamba atapendezwa sana kumalizia medani ya kabumbu akiwa katika ligi ya nchini England.

Mbali na klabu za nchini Italia na England kuonyesha nia ya kutaka kumsajili, napo nchini Marekani kuna baadhi ya klabu zimeonyesha nia kama hiyo, hivyo ni kusubiri na kuona ni wapi ambapo Zlatan atacheza soka lake baada ya kumalizana na PSG mwishoni mwa msimu uliopita.

AS Monaco Waahidi Kumsuka Upya Radamel Falcao
Wenger: Nipo Tayari Kupambana Katika Soko La Usajili

Comments

comments