Benchi la Ufundi la AC Milan limesisitiza halina mpango wa kumharakisha mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic kurejea dimbani, na badala yake ataendelea kuwa nje ya kikosi kwa lengo la kujiuguza.

Mshambuliaji huyo mkongwe, tayari ameshakosa michezo miwili dhidi ya Benevento na kisha Juventus.

Zlatan amekuwa nje ya kikosi cha AC Milan baada ya kupata jeraha la paja, Novemba 22 akiwa katika maandalizi ya kurejea kikosini, alipata jeraha lingine kwenye misuli na kuathiri mpango wa kurejea kwake, akilazimika kuuguza jeraha jipya.

Kwa mujibu wa chanzo cha habari za michezo cha Sport Mediaset, Benchi la Ufundi linaloongozwa na Stefano Pioli, halitarajii kumuharakisha mshambuliaji huyo wakihofia kumkosa kwa muda mrefu, hivyo wanahitaji kumpa muda zaidi.

Kwa mantiki hiyo, Zlatan huenda akarejea tena dimbani kwa zaidi ya majuma mawili yajayo, atakosa michezo dhidi ya Inter Milan, Benevento na Juventus itakayochezwa Januari 2021.

Msimu huu 2020/21, Zlatan mwenye umri wa miaka 39, amehusika kwenye mabao 11, katika michezo 10 aliyowachezea.

Haaland: Koulibaly ni mmoja wao
Afrika kusini: Serikali yarejesha masharti ya Covid-19