Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Croatia Zlatko Dalic amempongeza nahodha na kiungo wa timu hiyo Luka Modric kwa ujasiri wa kukubali kupiga penati ya pili wakati wa mchezo wa jana, licha ya kukosa mkwaju ambao huenda ungewavusha mapema dhidi ya Dennmark.

Modric alichukua maamuzi ya kuwa miongoni mwa wapiga penati tano zilizoamua safari ya Croatia kwenye fainali za kombe la dunia zinazoendelea nchini Urusi, baada ya kukosa mkwaju wa penati dakika ya 116, kufautia mshambuliaji Ante Rebic kuangushwa katika eneo la hatari na Mathias Jorgensen.

Dalic amesema Modric alionyesha ujasiri mkubwa wa kutaka aorodheshwe na kuwa miongoni mwa watakappiga penati tano, jambo ambalo kocha huyo amekiri alilikubali bila kinyongo.

‘Aliniambia nataka kuwa sehemu ya wapiga penati za mwisho, nilimkiubalia kwa sababu ninamuamini, na ndivyo alivyokwenda kufanya na alipata, baada ya kukosa mkwaju wa awali ambao ungetupeleka kwenye hatua ya robo fainali mapema.

“Yalikua maamuzi magumu kwangu na kwake pia, japo ninaamini kuna baadhi ya wenzangu hawakuliafiki katika nyoyo zao, lakini nilimuamuni Modric na alifanikisha nilichokikusudia kwake.

‘Alihitaji kuuonyesha umma wa mashabiki duniani, yeye ni nahodha asiyekata tamaa.” Alisema Dalic

Kuhusu mkwaju wa mwisho wa Croatia uliopigwa na kiungo wa mabingwa wa soka nchini Hispania FC  Barcelona Ivan Rakitic, kocha huyo amesema waliamini ingetokea kama ilivyotokea, kutokana na mchezaji huyo kuwa na umahiri mkubwa katika upigaji wa penati.

Dalic alisema: ‘Alikua shujaa wetu usiku huu. Alifanya kila kilichokusudiwa kwa kiasi kikubwa na walio wengi, sina budi kumpongeza Rakitic.’

Kwa ushindi huo Croatia watapambana na wenyeji urusi katika hatua ya robo fainali mwishoni mwa juma lijalo.

 

Video: Lebron James aimwaga The Cavs, atimkia Lakers na kitita kizito
Mashabiki Ureno wamhofia Cristiano Ronaldo