Uongozi wa klabu ya Birmingham City umemtangaza gwiji wa soka kutoka nchini Italia Gianfranco Zola kuwa meneja mpya wa kikosi chao, ambacho kinashiriki ligi daraja la kwanza nchini England.

Maamuzi ya kutangazwa kwa gwiji huyo ambaye aliwahi kuitumikia Chelsea wakiti akicheza soka, yemefanyika saa chache baada ya kutimuliwa kwa Gary Rowett.

Rowett alitimuliwa kazi kufuatia matokeo mabovu yaliyomuandama katika michezo mitatu iliyopita ambapo alikubali kupoteza dhidi ya Newcastle Utd kwa kufungwa mabao 4-0, na kisha alipokea kichapo kutoka kwa Barnsley cha mabao 3-0, na siku ya jumanne alifungwa 2-1 dhidi ya Ipswich Town.

Zola amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili na anaaminiwa kuleta mabadiliko makubwa katika kikosi cha Birmingham City, ambacho kimeshacheza michezo 21 katika ligi daraja la kwanza na kinashika nafasi ya nane kwenye mimamo kwa kufikisha point 34.

Zola amewahi kuvinoa vikosi vya klabu za West Ham na Watford zote za England, lakini hakufanikiwa kufikia malengo na mwishowe alitimuliwa kazi.

Zola anatarajiwa kufanya kazi na jopo lake la ufundi baada ya meneja aliyemtangulia kutimuliwa na wasaidizi wake ambao ni Kevin Summerfield, Mark Sale, Kevin Poole pamoja na Darren Robinson.

Aliyetobolewa macho na ‘Scorpion’ asimulia mkasa mahakamani
Chelsea Wajitanua Kileleni