Beki wa kati wa klabu bingwa nchini Italia Juventus FC Leonardo Bonucci, ameonyesha kukerwa na hatua ya kuzomewa na baadhi ya mashabiki wa nchi hiyo, alipokua katika majukumu ya kuitumikia The Azzuri kwenye mchezo wa ligi ya mataifa ya Ulaya dhidi ya Ureno uliochezwa mwishoni mwa juma lililopita.

Bonucci amesema hajapaendezwa na baadhi ya mashabiki waliokua wakimzomea wakati wa mchezo huo uliofanyika kwenye uwanja wa San Siro mjini Milan, hali ambayo amesema haionyeshi uzalendo wa kweli.

Beki huyo aliyesajiliwa tena Juventus akitokea AC Milan mwanzoni mwa msimu huu, anaamini hatua hiyo imetokana na chuki zilizojengeka miongni mwa mashabiki hao, ambao walichukizwa na maamuzi ya kuihama klabu hiyo ya mjini Milan.

Amesema linapokuja suala la kitaifa wataliano wote wanapaswa kuwa kitu kimoja, na jambo la kuzomeana linapaswa kubaki kwenye michezo ya ligi ambayo huusisha klabu na klabu.

“Sijapendezwa na kilichotolea, tulikua katika majukumu ya kitaifa, wote tulipaswa kuwa kitu kimoja kwa ajili ya taifa letu, wanapotokea baadhi ya watu wakaonyesha tofauti dhidi ya mchezaji mmoja ama sehemu ya wachezaji kwenye timu, inadhihirisha hatupo pamoja,” alisema Bonucci alipohojiwa na waandishi wa habari.

“Jambo la kuzomeana linapaswa kubaki kwenye ligi, huko kila mmoja ana haki ya kushabikia klabu anayoipenda, binafsi nikizomewa katika michezo ya ligi huwa sijali maana ninatambua mashabiki wa timu pinzani wanafanya wajibu wao, sio kwa upande wa timu ya taifa.”

“Ninajua mashabiki wa AC Milan wamekwazika sana na hatua ya mimi kuihama klabu yao na kurejea Juventus, lakini wanapaswa kutambua mchezo wa soka ni sehemu ya maisha yangu, ninapaswa kufanya maamuzi wakati wowote kwa kuzingatia maslahi yangu na familia yangu.”

“Nipo tayari kuzomewa nikiwa na jezi ya Juventus, lakini sio ninapikua na jezi ya timu ya taifa, halafu unabaini wanaofanya hivyo ni watu wa nyumbani kwenu, binafsi nimekereka sana.”

Katika mchezo dhidi ya Ureno ambao ulimalizika kwa sare ya bila kufungana, Bonucci alikua akicheza mchezo wake wa 84 akiwa na kikosi cha Italia tangu alipoitwa kwa mara ya kwanza mwaka 2010.

Mafanikio aliypyapata akiwa na timu ya taifa ni kucheza mchezo wa fainali wa mataifa ya Ulaya (Euro 2012) ambao walipoteza kwa kufungwa na Hispania mabao manne.

Hispania, Ureno kuishawishi Morocco 2030
Siwezi kuutazama mkanda wa mauaji ya Khashoggi, 'inauma sana'- Trump