Dar es Salaam, Tanzania. Mei 24, 2018, katika tuzo za Heshima za Afrika zilizofanyika hivi karibuni mjini Accra, Ghana – ZoomTanzania ilitunukiwa kama Kampuni Bora Zaidi ya Uajiri barani Afrika. ZoomTanzania.com inajulikana na wengi kama soko kubwa zaidi la mtandaoni nchini Tanzania likiwa na watumiaji zaidi ya 30,000 kwa siku, na limekuwa likiunganisha wanunuzi na wauzaji toka 2009. Jukwaa hili lina vipengele mbalimbali vya matangazo, kuanzia Nyumba na Makazi, Magari na Ajira, mpaka Vifaa vya Elektroniki, Vitu vya Nyumbani, pamoja na rajisi kubwa zaidi ya biashara Tanzania.

Akiongea baada ya kupokea tuzo hiyo, Mili Rughani, CEO wa ZoomTanzania na BrighterMonday Tanzania alisema, “Ni heshima kubwa kwetu kupewa tuzo hii. Ni utambuzi wa kazi kubwa ambayo ZoomTanzania imekuwa ikifanya ili kurahisisha upatikanaji wa fursa mbalimbali kwa Watanzania. Katika jitihada za kuboresha huduma zetu, tumeamua kushirikiana na jukwaa la mtandaoni la uajiri linaloongoza nchini, BrighterMonday.co.tz, ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kukabiliana na mahitaji ya mifumo ya uajiri yenye ubora yanayozidi kuongezeka.”

BrighterMonday hivi sasa ina nguvu kubwa katika soko la uajiri kupitia mtandaoni Tanzania, ikitoa huduma zote za uajiri, mtandaoni na kwa njia za kawaida. Muungano wa ZoomTanzania na BrighterMonday una nia ya kufanya mapinduzi katika soko la ajira Tanzania kwa kurahisisha utaratibu wa uajiri kwa kuwawezesha maafisa rasilimali watu kufanya maamuzi bora zaidi. Wataweza kufikia waombaji wengi zaidi wenye sifa na kuweza kuwafanyia usaili kwa urahisi zaidi, kupitia nyenzo zetu mbalimbali za kusimamia maombi ya kazi. Waombaji kazi pia watafaidika kwa kupata uwezo wa kutengeneza wasifu unaovutia, kupokea taarifa pale kazi zinapotangazwa na kupata ufahamu zaidi kuhusu utaratibu wa maombi ya kazi. Muungano huu unarahisisha na kuongeza ufanisi wa kuajiri au kuajiriwa.

Tuzo za Heshima za Afrika ni mpango wa tuzo wenye nia ya kutambua mafinikio yaliyofikiwa na wadau na viongozi mbalimbali katika biashara na mchango wao katika nchi zao, kwa huduma ambazo wametoa katika mazingira yao ili kusaidia watu wanaowazunguka.

Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Mei 25, 2018
Urusi 2018: Nani atabeba Kombe? Tuimulike Ufaransa

Comments

comments