Aliyekuwa rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, ambaye utawala wake uligubikwa na mivutano ameliambia jopo la mahakama linalochunguza madai ya rushwa dhidi yake kuwa kuna njama inayolenga kumchafua na kumfanya aonekane kama ni kinara wa ulaji rushwa.

Mwanasiasa huyo amesema kuwa kuna njama ya kumuangamiza kisiasa, kwakuwa amekuwa na wafuasi wengi ambao wanamuamini kuwa yeye ni kiongozi bora.

Aidha, Rais huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 77, alilazimishwa kujiuzulu wadhifa wa urais mwezi Februari mwaka 2018 kufuatia tuhuma za ufisadi wa hali ya juu uliodaiwa kutekelezwa naye kwa ushirikiano na maafisa wa chama tawala cha African National Congress (ANC).

Akijitetea, Zuma aliliambia jopo la Majaji linaloongozwa na jaji Raymond Zondo, kwamba madai hayo ya ufisadi ni njama ambayo imekuwepo kwa muda mrefu inayokusudiwa kumchafulia jina.

Hata hivyo, Zuma ameongeza kuwa mpango huo unatekelezwa na baadhi ya wakuu wa chama cha ANC, wakiwa na madhumuni ya kumuondoa kwenye siasa za taifa hilo la Kusini mwa Afrika.

 

Halima Mdee apewa mwezi mmoja kurudi Bukoba
Wanaoenda kutibiwa nje ya nchi kuanza kuchunguzwa