Chama Tawala Nchini Afrika Kusini (ANC) kimempa masaa 48 rais wa nchi hiyo Jacob Zuma kujiuzulu katika nafasi yake ya urais.

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini -SABC- na vyanzo vingine vya habari, vimesema kuwa hatua hiyo imefikiwa mara baada ya kuwepo kwa mlolongo wa mazungumzo yaliyofanywa na chama tawala nchini humo ANC.

ANC kilifanya mazungumzo ya kina na baadaye kutuma ujumbe wa watu wawili nyumbani kwa Rais Zuma jijini Pretoria kwenda kumfikishia ujumbe wa chama ana kwa ana ya kwamba achague moja ajiuzulu mwenyewe au chama kimng’oe madarakani.

Aidha, Chama hicho kimeona kuwa njia hiyo ni rahisi zaidi kumng’oa rais Zuma madarakani badala ya kusubiri utaratibu wa bunge ambao ungeweza kuwa mrefu na wenye madhara zaidi kwa chama cha ANC.

Hata hivyo, Kiongozi mpya wa ANC, Cyril Ramaphosa ndiye anayeongoza shinikizo la kumuondoa Zuma katika nafasi yake hiyo ya Urais, huku akiahidi kupambana na rushwa iliyokithiri na kukijenga upya chama hicho, wakati nchi hiyo ikielekea katika uchaguzi mwakani.

Video: Bashe adai hamjui Rais Dkt. Magufuli
Magazeti ya ndani na nje ya Tanzania leo Februari 13, 2018