Mahakama nchini Afrika Kusini imetupilia mbali rufaa iliyokuwa imewasilishwa na Rais Jacob Zuma kupinga kufufuliwa kwa mashtaka ya ulaji rushwa dhidi yake.

Zuma pamoja na maafisa wengine wakuu serikali walituhumiwa kupokea rushwa wakati wa ununuzi wa ndege za kivita, maboti na silaha nyingine.

Mwaka 2005 mfanyabiashara Shabir Shaik alituhumiwa kupokea rushwa kutoka katika kampuni inayouza silalaha ya Ufaransa kwa niaba ya Zuma lakini rais Zuma amekuwa akisisitiza kwamba hana hatia.

Mashtaka hayo yaliwasilishwa mara ya kwanza dhidi Jacob Zuma mwaka 2005 lakini yakaondolewa na waendesha mashtaka mwaka 2009 na kumuwezesha Zuma kuwania urais.

Mwaka jana Mahakama Kuu mjini Pretoria iliamua kwamba kiongozi huyo anafaa kujibu mashtaka hayo dhidi ya rais Zuma ambaye anamaliza muda wake wa uongozi mwaka 2019.

 

 

Katika kipindi ambacho amekuwa madarakani, amekabiliwa na kura ya kutokuwa na imani naye mara nane, na kunusurika.

Ndiye rais aliyenusurika majaribio mengi zaidi ya kutaka kumuondoa madarakani Afrika Kusini tangu kumalizika kwa utawala wa ubaguzi wa rangi mwaka 1994.

Polisi kufanya kazi bega kwa bega na viongozi wa makundi whatsApp, kudhibiti uhalifu
Nyumba zisizo na vyoo bora kutambulishwa kwa bendera nyekundu