Baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu wa 2020/21, Klabu ya Polisi Tanzania imetangaza majina ya wachezaji walioachwa na klabu hiyo yenye maskani yake makuu Mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Polisi Tanzania imetoa orodha hiyo, ikiwa ni siku moja baada ya Shirikisho la soka nchini TFF kutangaza kufunguliwa kwa dirisha la usajili wa wachezaji Wazawa na wale wa Kimataifa katika ligi zote.

Wachezaji waliotangazwa kuachwa na Polisi Tanzania ni Marcel Kaheza, Pius Buswita, Mohamed Kassim, Pato Ngonyani, Mohamed Bakari, Mohamed Yusuph, Ramadhani Kapele, Jimmy Shoji, Joseph Kimwaga, Eric Msagati, Hassan Nassoro, Emmanuel Manyanga na George Mpole.

Kwa idadi ya wachezaji wanaoachwa na Polisi Tanzania, ni dhahir klabu hiyo inasaliwa na wachezaji 19 na watasajili wachezaji wapya wasiopungua 8.

Wakati huo huo Polisi Tanzania imewarejesha wachezaji wote waliotolewa kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu, na wakati wa dirisha dogo.

Real Madrid kumuweka sokoni Eden Hazard
Mgodi wa Dhahabu Mara wapea siku 60 kulipa deni