Mjumbe wa kamati kuu ya halmashauri kuu ya taifa ya Chama cha mapinduzi (CCM), na waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakazi wa Singida kutafakari aina ya kiongozi wanayemtaka aiongoze Tanzania.

Waziri mkuu ametoa wito huo leo Septemba 15, 2020 wakati akizungumza na wananchi waliohuhudhuria mkutano wa kuwanadi wagombea wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya CCM kata ya Ilongero wilayani Singida.

“Uongozi wa nchi siyo jambo la mchezo, siyo jambo la kujaribiwa, wala haliendi kwa upepo na ushabiki. Ni lazima mkae na kutafakari ni nani anafaa kuongoza nchi hii,” amesema Majaliwa.

Wakati huohuo, Waziri mkuu amempokea aliyekuwa mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) wilaya ya Singida, Frank Petro Akunay ambaye ameamua kuhamia CCM.

Akunay amehamia CCM akiambatana na mkewe Betina Petro pamoja na mdogo wake Daniel petro akisema kuwa amerejea nyumbani kwani alikuwa CCM kabla ya kujiunga CHADEMA ambako ametoka sasa.

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Septemba 16, 2020
Tanzania: Mataifa 15 kupata kibali cha Uangalizi Uchaguzi mkuu

Comments

comments