Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kwa kushirikiana na Mkurugenzi wa jiji la Dar es Salaam, Zipora Liana, wamefanikiwa kudhibiti fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 12 za Mradi wa Ujenzi wa Stendi mpya ya mabasi ya Mbezi Luis jijini `dar es Salaam ambazo zilikuwa zitumike kuwalipa wakandarasi kama ziada kwa kazi ambayo haikufanyika.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU nchini Brigedia Jenerali John Mbungo, amesema udhibiti huo umefanikiwa kutokana na ufuatiliaji wa karibu kati ya wachunguzi na wataalamu wa ujenzi kutoka TAKUKURU.

Aidha TAKUKURU imeokoa na kurejesha fedha zaidi ya Shilingi Milioni 118 ambazo zilikuwa zimechepushwa kwa njia za udanganyifu kutoka shirika moja la kimataifa lisilo la kiserikali.

Brigedia Mbungo amesema kuwa TAKUKURU inatarajia kuzirejesha na kukabidhi kiasi kilichobaki cha Shilingi Milioni 172 ndani ya miezi mitatu kuanzi sasa (Hadi kufikia Januari 2021).

TAKUKURU imetoa wito kwa wote waliochukua fedha za umma kwa njia za udanganyifu au dhuluma kwa wanyonge, kuzirejesha kabla rungu la TAKUKURU halijawafikia.

Bonyeza link hapa chini kutazama video kamili

Ziara ya Pompeo Ulaya na Mashariki ya kati yazua gumzo
Waziri wa elimu Kenya afutiwa mamlaka ya kusimamia watumishi