Maafisa 15 wa kikosi cha ulinzi cha gavana wa Jimbo la Borno,nchini Nigeria Babagana Umara Zulum wameuawa katika shambulio lililotekelezwa na waasi wa kijihadi wenye mfungamano na kundi la Islamic State Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Vyanzo vya usalama nchini humo vimeeleza kuwa maafisa wanane wa polisi, askari watatu na watu wanne kutoka kundi la wanamgambo linalounga mkono serikali waliuawa katika shambulio hilo karibu na mji wa Baga kwenye mwambao wa Ziwa Chad.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa washambuliaji walishambulia msafara huo kwa bunduki za rashasha na silaha za kivita wakati msafara huo ulikuwa ukipita katika kijiji kilicho karibu na makao makuu ya Kikosi cha Pamoja cha Kimataifa (MNJTF), kinachoundwa na askari kutoka Nigeria, Niger, Chad na Cameroon.

“Gavana yuko salama na mzima, lakini maafisa 15 wa kikosi chake cha ulinzi wameuawa katika mapigano na magaidi,” kilisema chanzo kimoja.

Gavana huyo alikuwa amezuru Baga kama sehemu ya maandalizi ya kurudi kwa maelfu ya wakazi waliofukuzwa katika mji huo na wanajihadi mwaka 2014.

La mgambo linakaribia kulia Marekani
Togo: Waziri mkuu na serikali yake wajiuzulu