Nahodha na Mshambuliaji wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ inayoshiriki michuano ya Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ John Raphael Bocco amesema wapo tayari kwa mpambano wa mwisho wa kundi D dhidi ya Guinea utakaochezwa leo usiku mishae ya saa ne kwa saa za Afrika Mashariki.

Bocco, ambaye ameshindwa kuwa sehemu ya kikosi katika michezo dhidi ya Zambia na Namibia kufuatia majeraha yanayomkabili, amesema morari ya wachezaji wenzake ipo juu, hali ambayo inampa matumaini ya kuibuka na ushindi dhidi ya Guinea.

Amesema wanatambua mchezo utakua mgumu, lakini kila mmoja anaezungumza naye kambini amemuhakikishia watahakikisha wanapambana hadi dakika ya mwisho, ili kutimiza lengo la kupata alama tatu nyingine, baada ya kufanya hivyo dhidi ya Namibia waliokubali kichapo cha bao moja kwa sifuri.

“Wachezaji wamekuwa na morali kubwa mazoezini na wanajua kwamba Watanzania wanahitaji ushindi hivyo watapambana ili kufanya vizuri.”

“Kikubwa tunaamini kwamba mchezo utakuwa na ushindani mkubwa hilo lipo wazi ila tutapambana ili kupata matokeo chanya Watanzania watuombee ili tufanye vizuri.” Amesema Bocco .

Hata hivyo kuna hatihati kwa mshambuliaji huyo wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC akaukosa mchezo wa leo kwa kuwa yupo kwenye uangalizi maalumu wa jopo la madaktari pamoja na Ibrahim Ame ambaye ni beki.

Stars ipo kundi D ina alama tatu baada ya kucheza michezo miwili, imeshinda mmoja kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Namibia na imepoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Zambia kwenye mchezo wa ufunguzi.

Stars wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Bonamoussadi,Douala na mchezo wa mwisho wa Kundi D kwenye mashindano ya CHAN dhidi ya Guinea unatarajiwa kuchezwa leo Jumatano, Januari 27 saa 4 usiku Uwanja wa Reunification,Cameroon.

Majogoro anaamini Guinea wanakufa
Ndayiragije: Nimewahimiza wachezaji kupambana wakati wote