Waziri wa Viwanda, Geoffrey Mwambe, amesema shehena nyingine ya mafuta ya kula inatarajiwa kuwasili nchini Februari 17, mwaka huu,huku akitishia kuwafutia leseni mawakala wa bidhaa hiyo watakaobainika kuuza kwa bei kubwa tofauti na iliyopo sokoni.

Waziri Mwambe ametoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma kuhusu hali ya upatikanaji wa mafuta ya kula nchini.

“Kwa sasa tuna mafuta ya kutosha, lakini hizi meli mbili za tani 21,800 na nyingine 26,450, yoteyameshapakuliwa. Ukijumlisha na ambayo yapo, hatutarajii uhaba wa mafuta, kinachotarajiwa ni bei kuongezeka,” amesema.

Amewaangiza Wakurugenzi wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda, kufanya kazi na waagizaji wa mafutahayo, ili usambazaji ufanyike kwa usahihi.

“Kwa wale mawakala wakubwa, ninaomba nitoe onyo kabisa, bei ambazo zitakubaliwa kiwandanitunajua hadi bei ya mwisho, wakiuza bei kubwa kuliko ambayo kiwanda kimetoa na faida yao kulingana mwenendo wa soko, mimi nitawafutia leseni ya biashara,” amesema Mwambe.

Aidha Mwambe ametoa wito kwa wakulima kuzalisha kwa wingi, ili nchi ijitosheleze kwa mafuta kwa kuwa fursa hiyo ipo na kusisitiza kuwa  viwanda vikubwa 21 vilivyopo nchini, uwezo wake wa kuchakata mafuta ni asilimia 25 hadi 35 na vingi havina malighafi kutokana na uzalishaji mdogo.

Waziri huyo alisema Taasisi ya Utafiti wa Mbegu (ASA) na Taasisi ya Kilimo (TARI), zimefanya utafiti nakutoa mbegu bora ambazo zina uwezo wa kutoa mafuta mengi.

FIFA yabariki uchaguzi mkuu CAF
Habari kubwa kwenye magazeti leo, Januari 28, 2021