Wabunge 19 wa viti maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), asubuhi ya leo februari 2, 2021 wamewasili katika viwanja vya Bunge na kuendelea na kikao cha Bunge la 12 kilichoanza leo Jumanne, Jijini Dodoma.

Wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee wametinga mjengoni wakiwa wamevalia mavazi meusi huku Mdee akiwa amevaa barakoa kwa lengo la kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.

Itakumbukwa Wabunge hao tayari walishavuliwa uanachama na chama chao mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama chao.

Hata hivyo kabla ya kuanza kikao cha Bunge, Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Kazi na Wenye ulemavu, Jeniste Mhagama aliwaomba watoke nje kwanza.

Spika Job Ndugai ameomba wabaki nje kwanza na baada ya dua ameanza kuwaita akianza na wabunge watano wa kuteuliwa, kisha wakaingia wabunge watano wa  ACT.

Mwisho waliitwa wabunge 19 wa Chadema wakiongozwa na Ester Matiko na Cesilia Pareso huku Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya hawakuwa miongoni mwa walioingia mapema leo.

Mkude akataliwa Simba SC, hatma yake kujulikana leo
Azam FC: Tutaifunga TP Mazembe