Watu 17 wakiwemo maafisa watano wa Polisi wameuawa katika shambulio la silaha katika jimbo la Katsina, Kaskazini-magharibi mwa nchi ya Nigeria.
Misitu katika eneo la kaskazini-magharibi mwa nchi imethibitisha maficho ya wahalifu wanaojulikana kama majambazi ambao hushambulia, kuua, kuteka nyara wanavijiji na kuiba mifugo.
Jumatano Julai 20, 2022, Msemaji wa Jeshi la Polisi jimbo la Katsina, Gambo Isah alisema baadhi ya majambazi 300 waliokuwa wakiendesha baiskeli walishambulia kituo cha polisi karibu na kijiji cha Gatakawa, katika Wilaya ya Kankara na kuwaua maafisa watano wa Polisi.
“Tulipoteza maafisa watano wa polisi na walikuwa wakipambana kuzuia majambazi kufanya mashambulizi katika kijiji cha Gatakawa lakini kwa bahati mbaya nao wakashambuliwa na kupoteza maisha,” alisema Isah.
Aidha, inaarifiwa kuwa Jumanne Julai 19, na Jumatano Julai 20, 2022 katika mashambulizi mengine yaliyofanywa na kundi moja la majambazi katika kijiji cha Faskari, zaidi ya watu watisa waliuawa katika eneo hilo.
“Vijiji 4 vilishambuliwa kwa jumla ya watu watisa waliuawa, watu wasita kutoka kijiji cha Ruwan Goduya walikufa na mtu mmoja aliuawa katika kila vijiji vitatu vilivyoshambuliwa, na hao majambazio ambao baada ya shambulio waliiba ng’ombe na vitu vingine vya thamani,” alisimulia mmoja wa wakazi wa eneo la Katsina Musa Ado.
Majambazi katika ncvhi ya Nigeria hasa eneo la Kaskazini, wamekuwa wakifanya mashambulizi ya kila mara hasa jimbo la Katsina, wakitokea jimbo jirani la Zamfara ambako ndipo ilipo ngome yao kuu huku Serikali ya nchi hiyo ikisema inafanya jitihada za kukabiliana nao.
Iwapo nia kuu za magenge haya inaaminika kuwa ni mvuto wa faida, mamlaka ya Nigeria inahofia kuwa inajenga uhusiano na makundi ya wanajihadi, ambayo yameivuruga Afrika yenye idadi kubwa ya watu kwa miaka 13, huku wakiongoza uasi kaskazini-mashariki mwa nchi hiyo.