Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi linawashikilia watu 20 kwa tuhuma za kuwanyofoa watu sehemu zao za siri.
Mkuu wa Mkoa wa Katavi, Juma Homera amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, akieleza kuwa wanadaiwa kutumia mapanga na vitu vyenye ncha kali kukata nyeti za watu.
Akizungumza baada ya kumkabidhi Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Bejamini Kuzaga pikipiki yenye thamani ya Sh. 2.5 Milioni aliyoitoa kama mchango wake kwa jeshi hilo, Mkuu wa Mkoa alisema kuwa jeshi hilo pia kupitia oparesheni maalum limekamata lita 240 za pombe haramu aina ya gongo.
Kwa upande wake Kamanda Kuzaga alisema kuwa jeshi hilo litaendelea kuwasaka waharifu na kuwafikisha kwenye vyombo vya sheria. Alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa mchango wake na kuwataka wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi hilo katika kutokomeza uharifu.
Ibrahim Ajibu alimwa mshahara Simba SC
Ripoti: Kilichotokea baada ya Trump kutishia kutumia jeshi kuzima maandamano